
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) leo amehukumiwa adhabu ya kukaa nje miezi mitatu bila kujihusisha na kosa kama alilolifanya la kumtukana aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mnamo Desemba 14, 2015 katika kiwanda cha TOOKU Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External jijini Dar, Mhe. Kubenea alimtolewa lugha chafu Mhe. Makonda.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar chini ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Thomas Simba