
Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kuna ule unaopevusha mayai ‘Ovulatory Cycle’ na usiopevusha mayai ‘Anovulatory Cycle’. Aina hizi za mizunguko tutakuja kuziona kwa undani katika makala zijazo, lakini mzunguko unaopevusha mayai mwanamke anapata ute wa uzazi ambao unavutika na anaweza kupata ujauzito. Mzunguko usiopevusha mayai mwanamke hawezi kupata ujauzito ingawa katika mizunguko yote hiyo miwili mwanamke anapata damu ya hedhi kama kawaida. Mwanamke ambaye mzunguko wake hapati ute wa uzazi, hawezi kupata ujauzito. Hii inatokana na mabadiliko katika mfumo wake wa homoni. Ute wa uzazi umegawanyika katika makundi matatu. Ute mwepesi, ute unaovutika na ute mzito.
Mwanamke asiyepevusha mayai hawezi kupata ujauzito, hivyo hapati ute wa uzazi wengine hupata ute mzito…
GPL Mwanamke asiyepevusha mayai hawezi kupata ujauzito, hivyo hapati ute wa uzazi wengine hupata ute mzito…