Total Pageviews

WANAUME SOMENI....tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na tiba yake

KWANINI WANAUME HUISHIWA NGUVU ZA KIUME

Kuishiwa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kwa uume kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa au kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni au yote mawili kwa pamoja.ili mradi ufanisi katika kukamilisha tendo hilo haupatikani ipasavyo.

hatari ya kupungukiwa na nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri.Kulingana na tafiti za kitabibu wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa sana kwao kuliko hata wanaume walio chini ya miaka 40,hata hivyo siku hizi vijana wengi wana tatizo la kuishiwa nguvu za kiume.

Wanaume wenye elimu kidogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya nao wanakabiliwa na tatizo hili sana ,hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula cha kuongeza  nguvu za kiume,mitindo ya maisha wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo.Mazoezi ya mwili pia hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume.

inakadiriwa kuwa asilimia 50 mpaka 60 wenye tatizo la kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama pia wanaosumbuliwa na kiharusi,walevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani[testicles]katika ulevi sugu na kupoteza testosterone,pia wenye shinikizo la damu,magonjwa ya tezi,majeraha kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi,matumizi ya dawa za kemikali bila ushauri wa wataalam hudhoofisha damu kwenda kwenye uume.

 VYAKULA 10 VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME

 Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo

PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.



PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.
 CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.

KOMAMANGA
Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yanatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.


MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu.


MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya
mtu ajione ni mwenye afya njema.
VANILLA  
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni 
TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »