Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu juzikati jioni alitinga
nyumbani kwa Shilole na kufanikiwa kuwakuta wawili hao lakini katika
hali ya kushangaza, baada ya kuona kamera wakaanza kufanyiana vituko vya
kimahaba.
![]() |
| Shilole na Medy Music wakiperuzi kitu kwenye simu huku furaha ikitawala. |
Shilole
alionekana kumshikashika Medy huku dogo huyo aliyeonekana kuwa kama
kalewa akitoa ushirikiano.Katika meza iliyokuwepo sebuleni kulikuwa na
chupa za bia lakini mara kadhaa Shilole alionekana akinywa juisi huku
dogo akipiga maji, mazingira yaliyoonekana kuwa Shilole alikuwa
akimlewesha kwa makusudi kisha mambo ya ‘kuchi…kuchi’ yachukue nafasi.
![]() |
| Shilole na Medy Music hapa sijui wamegundua jambo gani la kushangaza. |
Akizungumzia
uhusiano wake na Medy, Shilole alikiri kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa
na akawataka wanaodai anambemenda wakidhani ni mtoto wakae kimya.“Huyu
ndiye laazizi wangu kwa sasa, ana kila sifa ya kuwa mume wangu na wala
siyo mtoto, ni mtu mzima kabisa tofauti na Nuh,” alisema Shilole kisha
kuendelea kumdekea jamaa huyo aliyeonekana kafa-kaoza kwa staa huyo.
Wakati Shilole akifanya yake, Nuh naye juzikati alitupia picha kadhaa
mtandaoni akiwa kimahaba na demu mkali aliyefahamika kwa jina la Erah
Erah anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
![]() |
| Mhaba mapya kati ya Shilole na Medy Music. |



